Chrome hukusaidia kufanya kinachowezekana kwenye wavuti. Chagua kivinjari chenye kasi na salama kutoka Google.
NUFAIKA ZAIDI NA GOOGLE KWENYE CHROME
• TAFUTA UKITUMIA GOOGLE - Tafuta na upate majibu kwenye Google kwa haraka. Tumia sauti yako kutafuta bila kugusa kifaa.
• LENZI YA GOOGLE - Tafuta unachoona karibu nawe ukitumia kamera yako.
• GOOGLE TRANSLATE - Gundua wavuti katika zaidi ya lugha 130. Tafsiri tovuti nzima kwa mbofyo mmoja.
VINJARI KWA USALAMA ULIO BORA ZAIDI
• HALI YA ULINZI ULIOBORESHWA - Vinjari bila wasiwasi ukitumia kiwango cha juu zaidi cha usalama wa Chrome.
• UKAGUZI WA USALAMA - Ondoa wasiwasi kwa kupata arifa hima za usalama.
• KIDHIBITI CHA MANENOSIRI CHA GOOGLE - Tunga na uhifadhi manenosiri kwa njia salama ili uingie katika akaunti kwa haraka na upate arifa manenosiri yako yakiwa hatarini.
TUMIA CHROME YAKO KWENYE VIFAA
• SAWAZISHA KWENYE VIFAA - Hifadhi vitu vyako (kama vile alamisho, vichupo na manenosiri) na uvifikie kwa urahisi unapoingia katika Chrome kwenye simu, kompyuta au kishikwambi chako.
• VIKUNDI VYA VICHUPO - Anzisha vikundi vya vichupo ili uwe na mpangilio kwenye vifaa.
• KUJAZA KIOTOMATIKI- Okoa muda unapoandika kwa kujaza kiotomatiki maelezo ya malipo, anwani na manenosiri yako uliyohifadhi.
Ilisasishwa tarehe
24 Jul 2025